UCHAWI WA HERUFI. ALIF - Dr BaBu Haji

Latest

Dr BaBu Haji

SWAHILI VERSION KWA TIBA ZA ASILI,UTABIRI WA NYOTA,UTAFSIRI WA NDOTO,KUONDOSHA ADHA YA MAJINI,MIKOSI,BIASHARA,MAPENZI,NGUVU ZA KIUME,UZAZI,KUMWITA ALIYE MBALI NA KUSAFISHA NYOTA,MUONE DR HAJI. ENGLISH VERSION MEET THE TRADITIONAL HEALER DOCTOR AND ZODIAC SIGN PREDICTOR

Dr Babu Haji

Dr Babu Haji
+255767393934/ +255657555550

Translate

Saturday, October 12, 2019

UCHAWI WA HERUFI. ALIF


MAAJABU YA ABJEDI
Herufi 28 za Kiarabu hutumiwa katika uchawi, na zinahusiana na uundaji wa viumbe mbali mbali, kama vile majini, upepo, radi na mamb mengi mbali mbali.
Alif ni kafara au ni ufunguo wa matumizi ya jina la allah ambalo ni ILAHI,AKBARU,ALLAHU.
Kwa mfano Qaf ina ashiria kun wa karim wa kitabi (kun fa yakun) hii ni elimu nzito sana haswa kwa madaktari wenyekuhitaji kukuza elimu zao na kuongeza kipato NK.

HERUFI YA KWANZA ALIF
Alif – ni jina au herufi yenye kumaanisha, Mtakatifu zaidi, Aliyetukuka,herufi hii ndiyo herufi ya mwanzo katika herufi zote na ndiyo herufi yenye nguvu kuliko zote.
Wakati una iandika Alif kwa shida yoyote inatakiwa uwe unasoma au unatamka maneno haya mpaka utakapo maliza kuandika,subhana Allah ya lailaha ilalah anta.

(a) Mwenye kusoma au kuitaja x1000 kila baada ya swala ya alfajiri atatajirika kwa uwezo wa Allah.

(b) Mwenye kuisoma x166600 laki moja na elfu 66 kila siku kwa muda wa siku 7 mfululizo atakua na uwezo wa kuongea na kiumbe wa aina yeyote miongoni mwa watu na majini.
(c) Alif huondoa ukosefu wa hifadhi yaani huleta fahamu na kuondoa tatizo la kusahau kama utaiandika mara 99 kwa zafarani kisha ukaitumia kwa kunywa na kunawa kichwa, hii huongeza akili hata kwa wasomi.
(d) Inavuta mapenzi kwa watu walio gombana mke au mme kama utaichora tarasimu yake na kisha kuizungushia manuizi na baada ya hapo ukaisomea herufi hiyo hiyo kisha ukatundika juu ya mti au ukazika katika moto yaani chini ya mafiga, hakika mapenzi yatarudi kwa kasi sana kwa uwezo wa Allah.                                                                     
(e) Inaunganisha watu katika mahaba na ina zuia mke au mume kuzini kama utaichora tarasimu yake na kisha kuizungushia manuizi na majina yenu wotw wawili kisha ukaisomea Alif x 666, kisha ukaloweka kama kombe na ukampa mwenzio akanywa katika chai, maji ya kunywa ni, hakika atakupenda kupita kiasi na hawezi kukusaliti hata siku moja.
(f) Inafungua hazina yani mali zilizo fichwa na watu wa kale au majini, na ina vumbua madini, ukiichora tarasimu yake na zafarani kisha ukaisomea mara 166600 kisha maji yake ukapaka usoni na umwaga katika hazina ilipo au ndani ya shimo la madini hakika madini yatakuja juu na kujiweka wazi.
                                                                                            (g) Ukii andika Alif x113 inahifadhi mali isiibiwe.

(h) ukiitumia vizuri herufi hii unaweza kujificha kwa adui au jambazi wasikuone, chora tarasimu yake kwa wino mweusi kisha ifunge na jumba la Buibui na uisomee Yasini aya ya kwanza hadi aya ya 9, isomee mara 9 kisha uwenayo hakika hutoonekana kwa mtu yeyote mwenye nia mbaya na wewe.

(i) Alif ina uwezo wa kufunga siraha ya adui isitoke hata kama ni kisu kisikuchome kama utaisoma wakati wa vita.
                                                                                              (j) Unaweza kupata sili kwa mtu yeyote kwa kutumia Alif kama utaisoma kwa wingi wakati wa kulala hadi usingizi ukupitie.

(k) Ina angamiza maadui kama utaisoma kwa wingi na kwa kutia manuizi, kazi hii ifanye usiku wa Ijumaa kuamkia jumamosi, na ubani wa kutumia ni miiat saila.

Marohani au watumishi wa herufi hii ni umma katika umma na wanafanya kazi za shari na kheri.

(l) Usiku wa alhamisi kuamkia ijumaa andika Alif x111 utapata utukufu na utapendwa sana na watu na utapata cheo na uta heshimika kwa watu

(m) Kupata mali nyingi au utajiri soma Alif x1000 kila asubuhi kabra hujaongea na mtu hakika utakua tajiri kwa uwezo wa Allah.

Ukiiandika x1000 siku ya alhamisi kuamkia ijumaa au ijumaa saa moja asubuhi au alhamisi katika karatasi pia huleta utajiri.



No comments:

Post a Comment