Kwanza
napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba mbingu na ardhi na kila kilichomo kwa
kunijaalia afya njema na kunijaalia uwezo wa kuwapa elimu hii ya ndoto.
Ndugu
msomaji wa kitabu hiki cha ndoto namba mbili
Katika Uislamu tumeambiwa
Ndoto ni sehemu ya unabii tulioachiwa, pia uislamu unaeleza aina kuu mbili za
ndoto yaani Ndoto zinazotokana na shetani na ndoto inayotoka kwa mwenyezi
mungu.
Pia Uislamu umeeleza ndoto ya kweli uotwa muda
gani (Mfano amesema bwana Mtume Muhammad (SAW), ndoto yeyote atakayeota muumini
kabla ya swala ya alfajiri, ndoto hiyo ni ya kweli), kwa ufupi ndoto ya kweli
ni ile mtu anayeota usiku wa manane akiwa hana msongamano wa mawazo na wala
huna janaba la hawala.
Uislamu umesema kuwa kama mmoja wenu ameota
ndoto nzuri basi amfuate mmoja wenu anayejua na amweleze ili apate maana yake.
Kama uislamu umeelezea vizuri kuhusu ndoto Je ndoto hutafsiriwaje?..
Ukiota ndoto yoyote katika wakati ulioelezwa
basi angalia hiyo ndoto kama inafanana na Aya yeyote ya Kuran anu Hadith Yeyote
ya Bwana Mtume. Hiyo itakuwa ndio maana yake:-
Mfano 1: Umeota umetumbukizwa kwenye Kisima, tafsiri yake ni
surat Yusuf... Yaani Ndugu zako wanataka kukutendea uadui, lakini kwa uwezo wa
Mwenyezi mungu hawatafanikiwa wanavyotaka na utakuja kuwa na uwezo wa mali na
mamlaka kuliko wao.
Mfano wa Pili: Umeota ndege amekudondoshea jiwe kichwani, Tafsiri
yake Surat fil... Unaonywa kuwa unafanya yaliyovuka mipaka hivyo utaangamia.
Mfano wa tatu: Umeota Ndege anaokuambia kitu, Tafsiri yake ni surat
Naml. Habari
anayokuambia ni ya kweli hivyo unatakiwa uifanyie kazi haraka.
Mfano wa nne: Umeota unakurupuka na ukaambiwa kiama! watu wengi wanakwenda
wasipopajua, Tafsiri yake ni kuwa unapewa Onyo kuna jambo linalomchukiza Mungu
unalifanya acha mara moja. kumbuka pale allah aliposema kuwaambia waovu
"Hakuna wanachokisubiri ila ni kiama ambacho kitawakuta Ghafla".
1.
Ukiota ulimi wako
umefungwa, ni dalili ya ufukara na maradhi.
2.
Ukiota una meno meupe na
mazuri, ni dalili ya ziada katika nguvu na mali ya daraja ya juu kwa watu wa
nyumbani mwake.
3.
Ukiota una meno ya dhahabu,
ukiwa ni mwenye elimu basi ndoto yako ina sifa nzuri,na ikiwa sio mwenye elimu
basi basi ni dalili ya shari na watu wako watapatwa na maradhi au kuangamia.
4.
Ukiota una meno ya fedha,
ni dalili ya kupata hasara katika mali yako,na yakiwa ni meno ya kioo ni dalili
ya umauti.
5.
kuota unalisha maskini,
utatoka kwenye majonzi na utapata amani kama ulikuwa na hofu.
6.
Ukiota unaswali katika
alkaaba, utapata baadhi ya watukufu na viongozi na utapata amani na kheri.
7.
Ukiota umekufa na kufufuka,
utafanya madhambi na utamuomba mungu msamaha.
8.
kuota unakufa bila
kuumwa, umri wako utakuwa mrefuu.
9.
Ukiota umekufa,watu
wanaombeleza na kukufanyia shughli za mazishi
dunia yako itakuwa nzuri lakini akhera yako imeharibika.
10.
kuota maiti inajiosha
yenyewe, watu wako watatoka kwenye majonzi na mali yao itazidi.
11.
kuota unaona sanda, ni
dalili ya zinaa.
12.
Ukiota sanda
imeveshwa lakini haijakamilika uvaaji wake
utatiwa kwenye zinaa lakini hutokubali.
13.
Ukiota umefungwa kwenye
sanda vilevile kama maiti
ni ishara ya kifo chako.
14.
kuota upo kwenye jeneza,
utajenga udugu na mtu kwa ajili ya mungu.
15.
Ukiota upo kwenye jeneza na
watu wamelibeba
utatawala na kupanda daraja na watu watakufuata kama ulivyowaona ndotoni.
16.
Ukiota umebeba maiti, utapata
mali ya haramu.
17.
Ukiota unampeleka maiti
sokoni, utapata mahitaji yako na faida kwenye biashara zako.
18.
Ukiota jeneza linapita
hewani, atakufa mtu mkubwa kama rais, mwanachuoni au yeyote mwenye daraja ya
juu.
19.
Ukiota umekufa na unazikwa,
utasafiri safari ya mbali na utapata mali.
20. kuota
umemfufua maiti
utamsilimisha mtu wa dini nyingine kuwa muislam au mtu muovu atatubia dhambi
zake kwako.
21.
Ukimuota dada yako
aliyekufa anaishi, utajiwa na mgeni kutoka safarini na utafurahi.
NDOTO ZA NYOKA
22. Nyoka katika ndoto anawakilisha mtu anayeishi
Bondeni, vilevile Nyoka katika ndoto ni ishara ya uadui kutoka kwa wakwe zako
au watoto au ni ishara ya uovu na wivu kutoka kwa majirani zako au jini mbaya.
23. Ukiota unamuona nyoka maana yake ni kwamba
utadanganywa na mkeo au mumeo.
24. Ukiota unapigana na nyoka ni ishara ya
kuwashinda au kuwapindua adui zako.
25. Ukiota unakimbizwa na nyoka ni ishara ya
uadui unaokujia kutoka kwa adui yako.
26. Ukiota umemuona nyoka mwenye vichwa saba ni
ishara ya wewe kutenda dhambi au makosa makubwa.
27. Ukiota unamuona chatu anakushambulia ni
ishara ya kwamba mwanamme au mwanamke mwenye uwezo ambaye ni adui yako
atakusumbua sana. Kama ukiota ameshindwa kukuumiza maana yake utapewa sifa za uongo.
Ukiota umemuuwa ni ishara ya kuwashinda maadui zako.
28. Ukiota nyoka amejikunja ni ishara ya kupatwa
na hatari au kifungo. Pia ni ishara ya kupata maradhi na kuchukiwa na watu.
29. Ukiota nyoka amelala maana yake ni adui
aliyelala hasa kwa mtu ambaye ni muovu.
30. Ukiota nyoka wa kwenye maji maana yake ni
kwamba utapokea msaada au utapata uamuzi kuhusu jambo lako.
31. Ukiota unafuga nyoka au unamiliki nyoka hiyo
ni ishara ya kupata uwezo au madaraka.
32. Ukiota nyama ya nyoka maana yake ni fedha za
adui au ni ishara ya wewe kupata furaha.
33. Ukiota umevaa ngozi ya nyoka maana yake ni
kwamba utamgundua adui yako.
34. Ukiota umemuua nyoka na damu yake ikakurukia
kwenye mikono yako maana yake ni kwamba utamshinda vibaya adui yako.
35. Ukiota umemwona nyoka anauliwa barabarani
hiyo ni ishara ya kutokea vita au magomvi.
36. Ukiota nyoka mdogo ni ishara ya matatizo kwa
mtoto wako au mtoto yeyote unayemhudumia au kumsaidia.
37. Ukiota unawinda nyoka maana yake ni kwamba
utamdanganya adui yako.
38. Nyoka mweusi katika ndoto ni ishara ya adui
yako mwenye nguvu.
39. Nyoka mweupe katika ndoto ni ishara ya adui
mnyonge.
40. Ukiota nyoka anakusemesha na anakuambia
maneno mazuri maana yake ni kwamba utapata bahati ya kukaa vizuri na adui zako
na utanufaika nao.
41. Ukiota nyoka anakusemesha na anakukaripia kwa
maneno makali hiyo ni ishara ya kwamba adui yako atakutesa na kukunyanyasa.
42. Ukiota umegeuka nyoka ni ishara ya kwamba
utatoka dini yako na kwenda dini nyingine.
43. Ukiota umegeuka nusu nyoka na nusu mtu huyo
ni ishara ya kwamba utafanikiwa kupunguza nusu ya nguvu za adui yako.
44. Ukiota umegundua ngozi ya nyoka ambaye
imetengenezwa kwa dhahabu maana yake ni kwamba utagundua mali iliyofichwa.
45. Ukiota nyoka anakumeza hiyo ni ishara ya
kupata madaraka makubwa ya uongozi.
46. Ukiota nyoka amekukalia kichwnai hiyo ni
ishara ya kupata heshima kubwa kutoka kwa watu wenye madaraka au viongozi.
47. Ukiota uwanja mkubwa uliojaa nyoka hiyo ni
ishara ya kwamba itanyesha mvua kubwa ambayo italeta madhara.
48. Ukiota nyoka mwenye pembe ni ishara ya kupata
mafanikio ya kibiashara.
49. Nyoka mweusi na chatu katika ndoto
wanaashiria viongozi wa kijeshi.
50. Nyoka wa majini ni ishara ya pesa au utapata
pesa.
51. Ukiota shamba lako limejaa nyoka ni ishara ya
kwamba utapata mazao mengi msimu huo.
52. Ukiota nyoka anaondoka nyumbani kwako maana
yake ni kwamba nyumba yako itavunjwa.
53. Ukiota umemuua nyoka ni ishara ya ndoa na
vile vile utawashinda adui zako na wote wanaokuchukia.
54. Ukiota unakula na nyoka meza moja maana yake
ni kwamba utatengana na rafiki yako.
55. Ukiota umemwona nyoka wa Jangwani maana yake
ni kwamba mtavamiwa na majambazi.
56. NDOTO ZA KUJISAIDIA HAJA KUBWA AU NDOGO
57. Mara
nyingi ndoto huja kama fumbo au mfano ili kuelewa maana ya ndoto uliyoota
yakulazimu ufahamu nini maana ya fumbo au mfano ulio uona katika ndoto.
58. Kuota
kitendo cha karaha au kuudhi haimaanishi kua hiyo ndoto ni mbaya. Mfano kuota
unajisaidia haja kubwa au ndogo
MAANA YA KUJISAIDIA
59. Kwanza
ifahamike kuwa kujisaidia ni tendo la kushusha au kuondosha takamwili zilizo
katika mwili, kwahiyo mwenye kuota anajisaidia haja kubwa au ndogo hii
inamaanisha kuwa mtu huyo ameshusha au atashusha mambo yenye kumuhemeza,
60. Hii
inamaanisha kuwa mtu huyo ataondokewa na matatizo na mambo magumu alionayo.
61. NB: Tofauti kati ya haja kubwa
na ndogo ni kwamba (1) Ukiota unajisaidia haja kubwa hii ina
maanisha utaondokewa na Matatizo makubwa na madogo ulionayo.
62. (2)
Ukiota unajisaidia haja ndogo inamaanisha utaondokewa na matatizo madogomadogo
tu ulionayo.
63. ALAMA
MUHIMU KATIKA NDOTO
64. FARASI=Anaashiria mtu;hali ya
maisha yake na roho yake pia (Mathayo 7:24-27 ,2Timotheo 2:20-21)
65. Samaki=
Watu
66. Majani
makavu= Kuchakaa
na kuwa mkiwa
67. Majani
mabichi= Neema
na ustawi
68. Ngazi=
Kuongezeka,kukua
mafanikio
69. Mbuzi=
Ulafi
70. Mbwa= uzinzi
71. Kondoo= Unyenyekevu,upole
72. Maji= neema,kurudhika, uadui, na
kuendelea
73. Daftari
na kalamu= Elimu
na mafunzo mbele yako
74. Kuku= papara na kuhangaikia mambo
yasiyokuhusu
75. Mwewe
mweusi= Mkuu
wa anga wa eneo
76. Paka= uchawi wa eneo
77. Nyoka= Njama,shetani,Ibilisi,Njama,uadui,jini.
78. Kipara= werevu,uzamani,wingi wa
maarifa
79. Nzige= uharibifu,hasa wa kipawa
au huduma au mazao
80. Asali= uponyaji,ulinzi,mvuto na
uzuri
81. Bundi=
mikosi, fitina, uadui
82. Fisi=
uchawi, mchawi, uadui
83. Unapoona
ulimi upo nje ya kinywa= roho ya usengenyaji,umbea,kugombanisha
84. Unapoota
unaumwa na kichwa= wachawi
na wanga wamekushambulia
85. Unapoota
unatembea lakini hufiki= Jambo unalolofanya sasa linakupotezea muda fanya jambo
jingine achana na hilo.
86. Unapoota
unaitwa na mtu usiyemjua= Roho ya mauti
87. Unapoota
watu waliokufa wanakuita= Maagano,mauti
88. Unapoota
unafanya mapenzi na ndugu yako wa kuzaliwa= Uhusiano wako na ndugu yako utaharibika muda
sio mrefu,pia utapata aibu
89. Unapoota
unalia na hakuna anayekufariji= Huna uhusiano mzuri na watu
90. Unapoota
ndugu wako wa karibu amekuja kukutembelea na kukuaga= Roho ya mauti ipo juu yake
91. Unapoota
upo mbele za watu wengi wanakusikiliza= Mwenyezi Mungu atakutukuza na kukujulisha
mbele za wengi au kupata cheo
92. Ukiona
nyumba/chumba kipya= Huashiria mawazo
chanya;huduma na maisha mapya katika eneo jingine jipya
93. Unapoota
upo uchi= Aibu;mambo
yako yatakuwa hadharani na kuonekana,kuwa mwangalifu katika siri zako kwa watu
94. Unapoota
unavuka mto lakini umelowana = Jaribu unalopitia utalishinda ila kwa taabu
nyingi,Lakini utavuka
95. Unapoota
umelala na mtu wa jinsia ambayo sio yako= Kuwa mwangalifu na aina ya mahusiano
uliyonaoyo yatapelekea kumkosea Mungu
96. Unapoota
mti mkubwa uliostawi sana= Mungu atakuinua na kukufanya mkuu au kazi zako zitakupa
kipato au kupanda cheo.
97. Unapoota
upo ziwani unavua samaki= ni dalili ya kipato, kuwateka watu ki hakili, na kama
unagombea cheo utashinda maana watu wata kusikiliza.
98. Unapoota
unakimbizwa na watu usiowajua kwa nia ya kukudhuru na ukawazidi mbio= Uwe mwangalifu kwani
shetani atatumia mapepo yake na wachawo,
pia ni dalili ya kwamba kunawatu wanakushambulia lakini hawatakushinda.
99. Unapoota
unakula lakini hushibi= Roho ya kutotosheka na kutapanya mali
100.
Unapoota umekatwa kichwa= Madalaka yako yamehamishwa
na kwenda kwa mtu mwingine.
101. Unapoota
unavalishwa joho= Mwenyezi
Mungu atakufanya kuwa mpatanishi kwa wengine.
102.
Unapoota shamba zuri limejaa mazao= Ni kipindi ambacho Mungu
atakurejeshea kwa wingi mafanikio yako
103.
Unapoota matunda yaliyoiva= Ni wakati wa mafanikio yako
tayari
104.
Unapoota mto mkubwa uliojaa mamba= Vikwazo na balaa vimewekwa
mbele yako
105.
Unapoota mlima mkubwa mbele yako= Jaribu mbele yako
106.
Unapoota umekufa= Ni taarifa kwako kwa mambo
uliyonayo yamekwisha.
NDOTO ZINAZO HUSU MAJI,NVUA,BAHARI,NK.
107.
UKuota mvua inanyesha ni baraka na kufanikiwa
mipango yako ya kimaisha, lakini ikiwa imenyesha kwenye nyumba yako tu nayo ina
maana hiyo kwako na kama ni mtaa au mji mzima basi ni heri na baraka kwa mji
huo, ikiwa ni ya mafuriko basi ni hatari na majanga katika sehemu husika. Ikiwa
maji yake machafu na umeyanywa hayo ya mvua basi ni kupata maradhi ya kulala
kabisa kwa muda mrefu.
108.
Kama utaona upinde wa mvua ndotoni nayo ni
baraka na amani lakini rangi nyekundu ya upinde ikitawala upinde huo ni
umwagaji damu kutokea au kama njano imetawala ni magonjwa au green ikitawala ni
neema na amani.
109.
Kuota mvua inanyesha kwa mtu aliye kwenye
safari inaonyesha vikwazo mbele ya safari yako vyaweza kukumba
110. Maji
ya mvua ukiota unayanawa kwa njia yoyote au unapata udhu nayo ujue ni heri na
msamaha mkubwa wa Mungu muumba na dalili ya ufanisi kiuchumi kwa mwenye hali
ngumu ya maisha. Kusamehewa na kupata uongof
111. Kwa
ufupi ukiota mvua ikinyesha kawaida basi ni amani na heri ikiwa inanyesha
kwenye ndoto asali, maziwa, na vitu vingine vizuri basi ni zaidi ya baraka na
heri kwa muotaji na watu wa karibu katika sehemu hiyo.
112. Kuota
mto ina maana ni mtu maarufu utakuwa naye karibu, kuota unaogelewa mtoni ina
maana uko na serikali karibu au utapata ajira serikalini mfanye kazi na
serikali, Kuota unaruka mto kutoka pande moja kwenda nyingine ya mto ni kuwa
unaokoka majanga na pia maadui unawazidi mbinu zao na kuwaepuka, pia mto
unaimanisha kupata safari muda wowote.
113. Kama
wewe utaota unageuka kuwa mto yaweza kuwa kifo chako kiko karibu,
114. ukiota
mto unasambaa mitaani na masokoni na watu wanaoga na kutumia maji kutawadha na
mambo mengine ujue mfalme muadilifu na mzuri mwenye kupenda watu atatawala na
ikiwa maji yanaingia mtaani na kuharibu majumba na mali za watu ujue kuwa
mfalme asiye muadilifu atatawala na kuumiza watu kiasi kwamba watakosa amani na
raha kutokana na mfalme huyo.
115. Ukiota
unaogelea kwenye mto mchafu jua ni dalili ya kuzama kwenye maasi na kutosikia
makumbusho unayoambiwa ya kuacha maasi
116. Ukiota
mto unatiririka kwenye nyumba yako ujue mali itaongezeka kwako na utakuwa
mwenye mali kukidhi mahitaji yako na ziada.
117. Kuota
radi kwenye ndoto inategemea umeota vipi, ikiwa radi tu bila mvua ni kuonyesha
kutokea majanga na hali tete
118. Ukiota
radi na mvua kwa pamoja ni kupata nafuu na mambo kuwa mepesi kuliko yalivyokuwa
na hii ni kuonyesha matumaini kuwa yanakaribia kwa hali unayokuwa nayo kama
mgonjwa anakaribia kupona , biashara inaelekea kuwa ya faida yaani kila pazito
panaelekea kuwa rahisi kwako.
119. Ukiota
unasikia mngurumo wa radi tu bila hata kuona mwale basi ni mauaji kutokea
katika maeneo na hali ya mtafaruku kutokea.
MUHIMU
Nipende tu kuwaambia na kuwa kila ndoto
inayoiota huwa na maana na pia huwa na tafsiri yake kutokana na mazingira
unayoishi pamoja na ufahamu wako kiroho.
Namaanisha kuwa unaweza ukaota ndoto
inayofanana kabisa na mtu mwingine lakini tafsiri zikatofautiana kutokana na
mtu na mtu na pia mazingira mnayoishi.
EE MOLA WANGU ULIE UMBA
MBINGU NA ARDHI NAKUOMBA UTUKINGE NA MABALAA YATOKANAYO NA MAJINI NA BINADAMU
NA UTUJALIE AFYA NA SALAMA YAA SALAMU ILI TUWEZE KUKUSHUKURU NA KUKUABUDU NA
UTUJAALIE MIONGONI MWA WAJA WAKO WEMA YA ALLAH.
ZAIDI WASILIANA NA
DR.HAJI KWA SIMU NO 0657,555550/767,393934/685,393934. Au tembelea blog,
http://hajibabuherbalistclinic.blogspot.com
shukran kwa kuniongezea maarifa
ReplyDeleteSAWA
ReplyDeleteshukrani kwa maarifa ila ukiota umepanda ngazi alafu ukaanguka lakini.hujaumia nini maana yake
ReplyDeleteukiota wazazi wako wamekufa inamaana gani
ReplyDeleteUkiota unawaona ng'ombe wamenona,wazuri,wanakula majani...ndoto hii ina maana gani?
ReplyDeleteUkiota unapaa yan up juu
ReplyDeleteUtapata pesa
Deletesamahn naomba kuuliza mm nimeota nimengoka meno yote yajuu hapa mbele inaashiria nn
ReplyDeleteUwadui
DeleteUtauguwa saanaaa
DeleteMimi nimeota napelekwa peponi nini maana yake
Deletenaomba msaada samahn
ReplyDeletenaomba msaadaa
ReplyDeleteMaana yake utafanikiwa
DeleteXamahani mm ni mwanafunzi na ninaota kuwa mtu anacheka bila sababu pia naota nyoka ananikimbiza ranging nyeusi ni kama chatu na mwingine ana ranging ya njano na nyeupe naomba unisaidie hata shuleni sifanikiwi inaniuma sana
ReplyDeleteVipi ukiota unapata hela nyingi ikoje hiyo
ReplyDeleteMaana yake amka kafanye kazi kwa bidii
DeleteAssalaam alaykum, mimi nauliza tafsiri ya ndoto ukiota unakula nyama mbichi. Ahsante
ReplyDeleteukiota rafiki yako kavaa nguo yako ya ndan? (boxer)
ReplyDeletenaomba msaada katafsiriwa
Hbr,mi nimekuwa nikiota ndoto za kutokuona Mara kwa mara Nini maana yake? Pia kuna wakati naota nafanya mapenz nikiwa na hisia Kali kbsa lakin kiuhalsia huwa Sina hisia za nmna hyo hata nikiwa na mpenz wangu, hii ina maana gan?
ReplyDeleteRafik Yang huyo Ni jini mahaba
DeleteUkiota umejifungua mtoto na tumbo laendelea kukuuma
ReplyDeleteUkiota na mihongo inaamaisha aje
ReplyDeleteNimeota nimepanda ngazi nilipofika mwisho nikataka kushuka lakini nikawa nashindwa, nikawa naomba msaada kwa rafiki yangu wa zamani msaada ili nishuke.
ReplyDeletemimi nimeota niko kwenyemeri lakini imepata ajali lakini nikafanikiwa kutoka na nika anza kuokoa watu maana yake sifahamu naomba nisahidie shekhe
ReplyDeletenimekua nikiota mara kwa mara ndoto moja nikiwa niko shuleni na naona watu walewale niliosoma nao je hii ndoto Ina maana gani
ReplyDeleteHupenda kazi ulio nayo ukafutwa ama ukapewa transfer, ama cheo ukapokonywa, in ishara ya kupungua kipato
DeleteNimeota nilikuwa nimejilaza wakati naamka nikamkalia panya mkubwa bila kukusudia nikainuaka haraka Ila hakunidhuru" hii ina maana gani
ReplyDeleteNimeota nimeingiliwa na mamba na kumzuia asiingie ndani hatimaye akaingia chumbani na kunin'gata mguu Kisha kushituka usingizini nn Mana yake
ReplyDeleteNimeota watu anaenda kuzika nikawa nataka nikapokezane kama ilivyo kawaida ila wakanifukuza .pia walikuwa wamevaa nguo nyeupe na nyekundu. Na walikuwa wanne tu.
ReplyDeleteHii Ina maana gani!?
Barikiwa sana
ReplyDeleteHOMON IMBALANCE (KUVURUGIKA KWA HOMONI)
ReplyDeleteHili ni tatizo linalowakumba wakina mama(wanawake) wengi ambalo husababishwa na kiwango kidogo cha hormone ya ESTROGEN.
VYANZO VYA KUVURUGIKA KWA HORMONE
👉Utoaji wa mimba
👉Uwepo wa sumu mwilini.
👉kutokula mlo uliokamili au mfumo mbovu wa maisha.
👉Family history(upungufu wa ongezeko ya homoni ya progesterone
👉mabadiliko ya mazingira au hali ya hewa.
👉uzito mkubwa
👉Msongo wa mawazo.
👉Kutofanya mazoezi.
👉Matumizi ya kisasa ya uzazi wa mpango.
👉Kukoma kwa hedhi.
Dalili za kuvurugika kwa homoni
👉Maumivu wakati wa tendo LA ndoa.
👉Kutoshika mimba.
👉Mzunguko wa hedhi kubadilika.
👉Kuongezeka uzito.
👉Kupungua hamu ya tendo LA ndoa.
👉Kupoteza kumbukumbu.
👉Hasira za Mara kwa Mara.
👉Damu kutoka nyingi wakati wa hedhi au kutoa damu yenye mabongemabonge
👉Uke kuwa mkavu.
👉kutoka jasho jingi usiku.
👉maumivu chini ya kitovu wakati wa hedhi
👉mzio wa vyakula/Allerg kuchaguachagua vyakula.
Madhara ya kuvurugika kwa homoni
👉kutoshika ujauzito kwa mda mrefu.
👉Mimba kuharibika Mara kwa Mara.
👉Kuwa mgumba.
👉U.T.I Mara kwa Mara.
👉Uvimbe kwenye via vya uzazi wa mwanamke.(fibroids)
👉kuziba kwa mirija ya uzazi.
👉saratani.
OFFICE ZETU ZIPO DAR-ES-SALAAM MIKOCHENI
Wasiliana nasi kwa tiba ya uhakika kwa asilimia 💯 kutoka Nature's..
Call/WhatsApp number +255752525797
Ukiota unafanya sherehe na ukiota kuna watu fulan wanakutesa
ReplyDeleteukiota upo kwenye dampo la takataka?inamaana gani?
ReplyDeleteUkiota nyoka yuko mbele yako anakusubiri ukakimbia na hakukupata
ReplyDeleteMm nimeota napandishwa jumba kubwa saaanaaa Kisha juu kabisa yajumba lenyewe mpaka nashika na hofu ya kuangalia chini
ReplyDeleteSikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe nikiwa nimesimama peke yangu bila mwili kusimama na mimi na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na mchawi huyu wa hodari Dk. ASUBUHI, baada ya kumueleza hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi akiniomba kuwa hatawahi. niache tena, miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa pia una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
ReplyDelete*penda uchawi
* kama unataka ex wako nyuma
* Acha talaka
*kuvunja mawazo
* huponya viharusi na magonjwa yote
* uchawi wa ulinzi
*Ugumba na matatizo ya ujauzito
Wasiliana na Dk DAWN kwa barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp: +2349046229159