MADHARA YA JINNI MAHABA NA TIBA YAKE
Jinni mahaba ni tatizo sugu
linalowasumbua watu wengi, na sababu kuu ya uwepo wa jinni huyo pia ni giza la
kiroho linaloundwa na akina mama bila ya wao kutambua.
Sasa anapofanikiwa
kumkamata mwanamke, alama ya kumtambulisha kuwa yupo huwa ni kutohisi hamu ya
kufanya tendo la ndoa na kujisikia kuwa mkali pale mume anapoulizia swala hilo
la tendo la ndoa, hali hiyo humpelekea mwanamke kua mkali maana wengi wao wenye
majini hawa huhisi uchungu au kuto kujiskia kufanya tendo hilo.
Wakati mwingine anakuwa na
majibu machafu na kero ili mradi tu wagombane halafu mume ageukie ukutani
au alale na suruali na hapo ndipo jinni huyo huja yeye na kufaidi tendo hilo
maana jinni huyu akikuta umeingiliwa na mwanaume huchukia sana.
Mpenzi msomaji wa kijitabu
hiki jinni huyu ni chachu ya kuvunjika kwa maelewano kati ya wawili wapendanao
na kinadada wengi tayari wameshakimbiwa na watu wao kwa sababu ya jinni huyu.
Pia katika mazingira
kama hayo mwanamke hujisikia raha zaidi ya ile anayoipata wakati akilala na
mwanaume wa kibinadamu na ndipo humaliziwa hamu yake ya kawaida kwa binadamu.
Wakati mwingine jinni huyu
husababisha maumivu sehemu ya tumbo hususan pale inapofikia wakati wa kutaka kufanya
mapenzi, jinni huyu pia husababisha mvurugiko wa vipindi vya mwezi na maumivu
wakati wa kuingia au kabla ya kuingia katika siku hizo, maana jinni huyu ukiwa
katika hedhi hawezi kukuingilia, japo wapo wakina mama wengine huingiliwa hata
wakiwa katika hali hiyo, ukiingiliwa ukiwa katika hali hiyo basi jua ya kwamba
jinni huyo sio jinni mahaba bali ni jinni maiti.
No comments:
Post a Comment